Rais Samia amesema Serikali itaendelea kukopa mikopo yenye tija ili kutekeleza miradi ya maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kukopa mikopo yenye tija ili kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itawanufaisha wananchi na kuwaletea maendeleo. Mhe Rais Samia amesema hayo leo tarehe 04 Januari, 2022, mara baada ya kupokea taarifa za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na